Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika barua iliyosainiwa na wanamichezo hao imesema: “Leo michezo haiwezi kubakia kimya ikitazama wanamichezo, wanawake, watoto na raia wasio na hatia wakiuawa na kumwagwa damu kwa njia ya kikatili kabisa huko Ghaza na Israel.”
Wachezaji wengi wametumia majukwaa yao kuonyesha mshikamano na watu wa Ghaza na kufariji maumivu yao. Aidha, wengi wameonyesha heshima yao kwa Sulayman al-Obeid, maarufu kama Pelé wa Palestina, ambaye aliuawa kishahidi na utawala katili wa Kizayuni mwezi Agosti uliopita.
Barua hiyo imetokana na wito wa wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa wanamichezo kutetea watu wanyonge wa Ghaza na kushinikiza kusimamishwa kwa timu ya Israel. Swala hili pia limejadiliwa kwa uzito katika mikutano miwili ya hivi karibuni ya FIFA.
Alhamisi, serikali ya Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani aliyeelemewa na kushindwa, ilitangaza kwamba haitaruhusu hatua hizi dhidi ya Israel kupita bila majibu, na kwamba daima itajitahidi kuzuia kusimamishwa kwa Israel katika Kombe la Dunia la 2026.
Cha kusikitisha ni kwamba licha ya mauaji ya halaiki yanayoendelea katika vita vya Ghaza, timu za Israel zimeendelea kushiriki kwenye mashindano ya FIFA na UEFA. Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya afya ya Ghaza, zaidi ya Wapalestina 60,000 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wanyonge wa Ghaza.
Chanzo: The New York Times
Maoni yako